Usikubali ngono ikatishe maisha yako. Weka malengo, timiza ndoto zako na UCE |
KUWEKA NA KUTIMIZA MALENGO
Utangulizi
Kila
mtu duniani hutumia muda mwingi kutafakari kuhusu maisha yake ya sasa na
baadaye. Isitoshe kila mtu anatamani kubadili mojawapo ya jambo katika maisha
yake. Yawe maisha ya kifamilia, marafiki, uhusiano au kipato. Inawezekana
kubadili jambo. Hatua ya kwanza ni kuweka malengo juu ya hilo jambo.
Kuweka
malengo ni utaratibu rasmi wa mipango unaozingatia kuchagua, na kupanga hatua
kwa hatua katika kufanikisha jambo. Lengo la somo hili ni kutoa elimu juu ya
kuweka na kutimiza malengo yako (sehemu ya I) katika maisha kwa ajili ya kuwa
na:
- Maisha
yenye afya
- Mahusiano
yenye afya
- Kazi na
wajibu
Faida za kuweka
malengo
- Kufanikiwa
zaidi katika maisha
- Kuboresha
mafanikio kiujumla
- Kuongeza
motisha ya kufanikiwa zaidi katika maisha
- Kuongeza
fahari na furaha katika mafanikio yako
- Kuongeza
kujiamini na kukua kwa utu wa mtu
- Kuondoa
mtazamo unaokurudisha nyuma na kukusababishia kukosa furaha
- Kupungua
kwa msongo na hali ya wasiwasi uliopindukia zaidi
Kuweka
malengo ni njia iliyowafanikisha wafanyabiashara wengi, wanamichezo
(wakimbiaji) na kadhalika. Kuona mafanikio ya malengo yako hukuza kujiamini
zaidi na kujenga imani ya uhitaji wa kutimiza malengo ya juu zaidi na magumu.
Kuchagua
lengo sahihi la kuanza nalo wakati mwingine ni vigumu. Lengo huanzia na jambo unalotaka
kufanikisha na unataka kuyaendeshaje maisha yako. Hili ni la msingi kwani lengo
hutoa dira ya muda mrefu, na motisha wa muda mfupi. Humsaidia mtu kutoa
kipaombele na ujuzi unaomsaidia kupangilia rasilimali alizonazo. Unaona mbali
katika lile lililoonekana awali kuwa jitihada zisizokuwa na maana.
Malengo
huwekwa kwa madaraja mbalimbali. Maswali ya kujiuliza ni:
- Unataka
kufanya nini na maisha yako?
- Unataka
kufanikisha nini?
Baada
ya kujibu maswali hayo, unayavunja katika makusudio madogo madogo yatakayokusaidia
kutimiza malengo ya maisha. Kisha uyafanyie kazi.
UCE team haifungwi na umbali, iwe mlimani, bondeni porini, tutakufikia kukuelimisha. Pichani ni Afisa uhamasishaji wa UCE Mr Mgina akitoa semina kwa wanafunzi wa Wasa Sekondari |
Madaraja ya Kuweka
Malengo
- Afya: Je unataka kuwa na afya ya aina gani kimwili,
kiakili, kijamii na kiroho?
- Mtazamo:
Upi mtazamo wako wa kimaisha?
- Kipaji /
karama: Je una kipaji gani?
- Elimu / Ujuzi:
Je ungependa kujiajiri au kuajiriwa?
- Familia: Je
ungependa kuwa mzazi wa aina gani?
- Fedha: Je
ungependa kuwa na kipato cha aina gani? Katika umri gani?
- Starehe: Ungependa
kuyafuraiaje maisha yako?
Kupanga na
Kuweka Malengo
Je
ni mara ngapi umefanya uamuzi juu ya kisababishi cha jambo na hukuweza
kulifuatilia? Isitoshe tatizo la wengi wetu tumekuwa tukiweka malengo yale yale
kila siku na kila mwaka ambapo hatukuwai kufanikiwa. Isitoshe kama tumefanikiwa
kwa nini kuendeleaza hayohayo tu kila mwaka?
Jifunze
kuweka malengo ya miezi sita, mwaka, miaka mitano, au miaka kumi. Malengo yako
yawe yenye kuleta mafanikio, unayoyafurahia, yenye kuzingatia tarehe, muda na
kiasi / kiwango ili kuweza kupima mafanikio ya malengo yako. Zingatia kutoa
kipaombele katika kuchagua lengo la kuanza nalo, yaandike malengo yako, hatua
uzipitiazo na yale uyafanyayo katika kutimiza malengo yako. Yaweke malengo yako
katika mambo madogo madogo utakayoweza kuyatimiza na kuyamudu. Kumbuka ili
uweze ktutimiza malengo yako kuwa na nidhamu ni jambo la msingi.
Unapofanikisha
lengo pata muda wa kujipongeza. Kutokana na ulilotimiza panga lengo lingine gumu
kidogo ya lile ulilofanikisha. Iwapo kuna funzo ulilojifunza kutokana na lengo
ulilofanikisha na unaona umuhimu wa kubadili jambo kwa malengo yajayo fanya
hivyo. Kama unahisi kukosa ujuzi katika malengo panga lengo la kutatua hilo mf.
Ongeza lengo la kupata ujuzi. Kumbuka malengo ni mtumwa wako na sio bosi wako.
Mratibu Mipango UCE Mr Lema , katika semina Ilula , ukanda wa Mazombe |
Mfando wa
Jedwali la Kupanga Malengo
Aina / Eneo la
Lengo m.f. Afya n.k
|
Faida za Lengo
Husika
|
Mchakato /
Ufunguo
|
Muda
|
Rasilimali
|
Matokeo
|
Toa
maana ya lengo lako, liandike kutokana na mpangilio na kipaombele
|
Orodhesha
faida utakazopata kwa kufanikisha lengo lako,
Jambo
gani litakufanya uwe mwenye furaha?
|
Hatua
zipi unatakiwa kufuata ili kutimiza lengo lako,
Je
utaanza na hatua ipi?
|
Andika
muda wa kuanza na utakaohitajika katika kulitimiza lengo lako
|
Andika
mahitaji yanayohitaji-ka katika kulitimiza lengo
Je
utazipata wapi?
|
Umefanikisha
nini?
Wapi
umekwama, na zipi sababu za kufanikiwa au kukwama?
Je
lengo lako litaleta athari gani katika maisha ya sasa na yajayo?
|
Kupanga Malengo Kunapofanyika Kimakosa
- Kupanga malengo ya matokeo pasipo kupangilia
utekelezaji wake hatua kwa hatua
- Kupanga malengo yasiyo na uhalisia kwani hakuna
jitihada za kuyatimiza
- Kupanga malengo yasiyoleta changamoto wala
faida inayoonekana
- Kutokuwa na mpangilio wa lipi lianze na lipi
lifuate
- Kupanga malengo mengi kwa wakati mmoja
Kicheko cha kiwango cha lami kwa mwanafunzi wa Nanenane sekondari Morogoro baada ya kufanya maamuzi ya kusubiri kwa kusaini kadi ya UCE. |
Zingatio
- Tafakari na jenga taswira ya maleongo yako
- Fikiria yapi yanaweza kukwamisha malengo yako
- Ainisha na bainisha mambo yatakayokusaidia
kutimiza malengo yako
- Pitia mara kwa mara malengo yako
- Jiwekee yapi ya kufanya na yasiyo ya kufanya
(Do’s and Don’ts)
- Jifunze kutawala muda wako vizuri (time
management) kwa kuoorodhesha yale yanayoiba au kupoteza muda wako
- Jifunze kutawala msongo katika hatua zote za malengo
yako
- Usiweke malengo madogo kwa kuhofia kushindwa
- Ni vyema kujua kushindwa kutimiza lengo
haijalishi sana iwapo kuna funzo umejifunza katika hilo lengo
- Kumbuka malengo yako yawe kwa yale unayotaka
kufanikisha katika maisha yako kwani mafanikio huja pale unapofanya kwa
ajili ya ustawi wako
Wanafunzi wa Mbalali sekondari mkoani Mbeya wakifurahia maamuzi yao ya kusubiri. INAWEZEKANA |
Karibu UCE Taanzania ujifunze mengi juu ya kulinda na kuimarisha afya |
Mtayarishaji / Mwezeshaji
Kazi hii imetayarishwa na kufundishwa Mr. Isaac S. Lema Mratibu Mipango UCE Tanzania
Kitaaluma: Mshauri (Professional Counsellor) Shahada ya ushauri toka chuo kikuu cha Tumaini Iringa
Tabibu Msaikolojia (Clinical Psychologist) shahada ya uzamili toka chuo kikuu cha Muhimbili Dar es Salaam;
Mawasiliano: Namba ya Simu: 0713 778808, 0764 345 318 Barua Pepe: lemaisaac@yahoo.com
Posted by Eng Nguki Herman. UCE Morogoo Regional Coordinator.
O763639101/ ngukiherman@ymail.com
www.ucetanzania.org