KWANI KUNA TATIZO? |
Kama nakusikia vile, karibu bhana tuwe wawili nje huku. |
Katika mizunguko yangu ya siku zote, huyooooooo hadi
hospitali ya mkoa wa Njombe maarufu kama
Kibena. Wakati nimekaa nje ya hospitali kando ya barabara nikamuona mama mmoja
(sio mkubwa sana, ni binti kijana) ambaye alikuwa mjamzito. Alikaa chini kabisa
kwenye nyasi huku akiwa mpole na akionekna kutafkari na mwenye mawazo mengi
sana. Kiufupi ilionekana kuna kitu kinamuumiza kichwani kwake, au anamaumivu ya
mwili, si unajua tena hawa ndugu zetu wakiwa katika hali hiyo complications
kibao.
Baada ya muda mfupi watu wakatokea hospitalini kuja upande wa
barabarani. Ni kijana mmoja na binti mmoja ambaye alikuwa mjamzito pia. Bila
shaka walikuwa mtu na mkewe kwa maana niliona Yule mkaka kamshikia mkoba huyu
dada, pia kamshika mkono huku wakiwa wanatazamana usoni kwa bashasha na
matabasamu ya kukata na shoka. Kha, nikajua ni mimi tu ndio nilikuwa nawangalia
wale watu kama sehemu ya tuition, kumbe hata yule dada aliyekaa kinyonge pale
chini alikuwa anawakodolea macho vizuri tu. Muonekano wa wawili hawa ulitoa
picha ya moja kwa moja kuwa wanaishi maisha ya furaha na walijipanga vya
kutosha, tena hawajutii maamuzi yao na matokeo yake. Yule dada pale chini
liendelea kuwaangalia kwa uchungu huku machozi yakimlengalenga (sina hakika
kama ni Kiswahili sahihi), aliwangalia hadi walipovuka barabara na kuendelea
kuwasindikiza kwa macho hadi walipoingia kwenye gari la kuelekea Njombe mjini.
Kisha akajiinamia chini huku ameshika shavu lake.
Mimi kama kijana nilijiuliza maswali mengi mepesimepesi na
kujijibu mwenyewe. Kwa mfano huyu mama hapa chini tena akiwa kachafuka na vumbi
huenda kaolewa lakini mumewe hajuwi majukumu yake kwa matokeo ya kile ambacho
alikifanya yeye mwenyewe. Au yamkini akawa hii mimba kapewa na mtu ambaye
hajamuoa bado hivyo mhusika kakataa kushughulikia lolote nakadhalika, au
pengine jamii nzima inayomzunguka imemtenga kwa mfumo fulani.
Ndugu zangu mama mjamzito mwenye msongo wa mawazo sio tu huathiri mfumo wa kawaida wa maisha
yake, lakini pia huathiri afya ya mtoto tumboni nap engine kumzaa motto mwenye
afya mbovu ya mwili au akili au vyote kwa pamoja. Mvulana ukikurupuka kwa
kuendeshwa na hashiki za mwili kasha kumdandia kwa pupa huyo uliyemshawishi kwa
pesa zako, unatengeneza bomu ambalo litakulpukia hapahapa duniani au hata ile
siku utakaporudi kwa yule aliyekuleta duniani.
Mfano hebu fikiria mama mjamzito ambaye kaolewa na yuko na
mumewe nymbani halafu usiku tumbo limuume kidogo, utasikia:
Mama : We baba kijacho, amka bhana mwanao kanipiga teke
tumboni hapa, linauma.
Baba : Oh, pole my
love, kwahiyo ngoja nimpigie rafiki yangu aje na tax twende hospitali.
Mama : Hapana acha tu
usiku sahizi, nitajitahidi kuvuilia tutaenda hata asubuhi.
Baba : Hapana, plz,
au tumpigie simu Dakitari aje akucheck hapahapa nyumbani.
Mama : Mhhh, usiku
wote huu, usijisumbue, acha tu mume wangu.
Baba : Haya mama,
basi ngoja tukae wote, silali hadi muanze
kulala wewe na kijacho wangu.
Mama : Hahaaa, acha
bhana, unadhani tumbo lenyewe linauma sana basi, nilitaka tu uamke nikusikie
kidogo baba kijacho waangu.
Baba : Duh, jamani haya mama. Minahamu na huyo
kijcho kama nini, sijui katakuwa kajogoo,au ndio mama ndio atajipatia mke
mwenza,, teh, heh, (anacheka huku akimbusu tumboni mkewe). Akizaliwa
nitamwambia ulimsingizia kuwa kakupiga teke kwa ndani kumbe ulitaka kusikia tu
sauti ya baba yake. Haya mama, lala basi nikufunike shuka … …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Umeona haya majadiliano? YANA AFYA, RAHA nakadharika.
Hebu tuwe wakweli. Dada ambaye kapewa mimba na mtu ambaye
hajamuoa bado. Hapo nyumbani wamemdongoa hadi basi, wamemsondea dole hadi basi,
(hadi huyo motto anajiuliza kwani huko nje kuna vita?) tumbo likiuma usiku
anamuamsha nani? HAKUNA KITU ZAIDI YA KUJIONA MKOSAJI NA KUMCHUKIA MTOTO ANGALI
YUKO TUMBONI. Kwa bahati mbaya mtu ambaye hayajamkuta, anaona ni kitu cha
kufikirika nay eye hakiwezi kumkuta wakati hataki kubadilika. Huo ni mtazamo wa
mtu mjinga. Maana mwerevu hujifunza kupitia matatizo ya watu wengine, lakini
mjinga haamini hadi yamkute yeye, ili werevu wajifunzie kwake kama sample
space.
Badilika na uchukue hatua leo, kama ulishakosea basi usirudie
tena, na kama Mungu amekuepusha hadi sasa, basi usifanye makosa kwenye kufanya
maamuzi. Fanya uchaguzi sahihi, funga ndoa halali, furahia wakati wa ujauzito
wako/ wa mkeo kwa raha zenu. Inawezekana…
Kwa kijana ambaye una malengo mwngiiiiii, itumie UCE Tanzania ikusaidie kuweka mikakati thabiti ya maisha yako n kamwe huwezi kujutia. USIFANYA NGONO KABLA NA NJE YA NDOA. TRUE LOVE WAITS………….Tafakari njema
Ukisikia UCE wanaongea na wanafunzi au wtu fulani, fanya hima uwepo ili kujichotea maarifa ya kuishi maisha yenye afya. |
Maelfu ya vijana mwameshafikiwa na team ya UCE hata kwako twaweza kufika. Karibu tujifunze pamoja, |
Eng Herman Nguki
UCE Tanzania Volunteer
+255 763 639 101/+255 679 639 101 /ngukiherman@ymail.com
Ngukiherman.blogspot.com / ucetanzania.org /uceglobal.org